KUFUNGULIWA KWA AWAMU YA TATU YA UDAHILI.
KUKAMILIKA KWA AWAMU YA PILI YA UDAHILI NAKUFUNGULIWA KWA DIRISHA LA UDAHILI
AWAMU YA TATU
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inatangaza kukamilika kwa awamu ya pili ya uhakiki wa sifa za waombaji waliodahiliwa na Taasisi za Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo 2018/19. Majina ya waombaji waliochaguliwa katika awamu ya pili yameshapelekwa kwenye vyuo husika kwa ajili ya kutangazwa.
Tume pia imefungua dirisha la maombi awamu ya tatu kuanzia tarehe 24 hadi 26 Septemba 2018 ili kuruhusu makundi yafuatayo kuomba udahili:
Waombaji waliokosa nafasi kwenye awamu ya kwanza na ya pili;
Waombaji wa kidato cha sita na stashahada walioshindwa kuomba katika awamu zilizotangulia;
Waombaji waliomaliza mitihani ya “Cambridge” mwaka 2018 na matokeo yao yameshatoka; na
Waombaji waliokuwa wamedahiliwa miaka ya nyuma na kuacha au kukatisha masomo.
Aidha Tume inapenda kusisitiza kuwa utaratibu wa kutuma maombi ni ule ule wa kutuma maombi moja kwa moja vyuoni kama ilivyokuwa katika awamu za Udahili zilizotangulia. Waombaji wote wanakumbushwa kuwa masuala yote yanayohusiana na udahili yaripotiwe moja kwa moja kwenye vyuo husika na siyo
TCU.
Imetolewa na
Katibu Mtendaji
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania
24/09/2018